KWELI JACK PATRICK ALIYEKAMATWA NA MADAWA YA KULEVYA CHINA NI MPENZI WANGU - JUX

0 comments

MALOVEE! Baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu, staa wa Bongo Fleva anayetamba na wimbo wake wa Nitasubiri, Juma Khalid ‘Jux’, kwa mara ya kwanza amevunja ukimya na kufungukia penzi lake na modo anayedaiwa kufungwa nchini China kwa msala wa madawa ya kulevya ‘unga’, Jacqueline Fitzpatrick Cliff ‘Jack Patrick’.
Staa wa Bongo Fleva anayetamba na wimbo wake wa Nitasubiri, Juma Khalid ‘Jux’.
Jux ambaye anasoma nchini China huku akifanya muziki wa Bongo Fleva, alifunguka hayo juzikati katika ‘exclusive interview’ aliyoifanya na mwanahabari wetu alipokuwa mjini Kahama alipokwenda kwenye Serengeti Fiesta 2014.
Akijibu swali la mwandishi wetu lililomtaka afungukie penzi lake na Jack ambalo alikuwa akichengachenga kila alipotakiwa kutoa ufafanuzi na vyombo vya habari, Jux alianza kwa kukiri kwamba mrembo huyo alikuwa mpenzi wake na walidumu kwa takriban miezi saba kabla hajakutwa na msala wa madawa ya kulevya.
Jacqueline Fitzpatrick Cliff ‘Jack Patrick’.
Alisema tangu aanze kuyajua mapenzi, Jack alikuwa ni mwanamke wa pekee kwake ingawa wakati anapatwa matatizo walikuwa wametibuana kwa kipindi cha wiki mbili.
“Nilisikitika sana niliposikia amekamatwa kwa madawa ya kulevya, nilikuwa sijui kama anafanya hiyo biashara na kinachoniumiza zaidi ni kwamba nilikuwa najua yupo Bongo na nikajua tutaonana maana mimi nilikuwa Bongo wakati huo,” alisema Jux.
Alipoulizwa kama ana taarifa za Jack kufungwa miaka sita jela kama ilivyoripotiwa wiki iliyopita, Jux alisema hana taarifa hizo.“Kiukweli sijazipata habari hizo labda nitakapoenda tena China ndiyo nitajua kupitia kwa mwanasheria wake maana kwa sasa hajanipa taarifa na hana namba yangu ya simu ya hapa,” alisema Jux.
Jux akiwa na Jack Patrick.
Jack alikamatwa Desemba 19, mwaka jana akiwa amebeba madawa ya kulevya aina ya Heroin yenye uzito wa kilo 1.1 katika Uwanja wa Ndege wa Macau akitokea jijini Bangkok nchini Thailand kuelekea Guangzhou, Mji Mkuu wa Jimbo la Guangdong Kusini mwa China.

TAZAMA PICHA ZAO WAKIWA CHINA KIPINDI FLANI

Read More »

Jokate Na Vanessa Mdee Katika Beef Zito Kisa Penzi La Ommy Dimpoz !

0 comments
Ommy Dimpoz na Jokate
Latest celebrities' gossip ni kuhusu Jokate Mwegelo ambaye pia ni actress, singer, designer and presenter kutoka kimapenzi na Ommy Dimpoz ambaye ni star wa Bongofleva.
Habari zaidi zinasema kuwa Jokate na Ommy Dimpoz wamekuwa wapenzi kwa muda sasa ila kwa siri kubwa ikidaiwa wote hawakuwa tayari kuweka uhusiano wao hadharani na media kuanza kuwafuatilia. Inadaiwa pia kuwa Ommy alikuwa anatoka kimapenzi na Vanessa Mdee lakini baada ya Vanesa kugundua kuwa Jokate anamzunguka zikawa haziivi tena na huchekeana kinafiki tu wakikutana in public. Kwasasa Jokate na Ommy wanaliendeleza libeneke la huba kwa siri ingawa gossip mongers tayari wameshawawahi !. Habari zinaingia ndani zaidin kwa kusema kuwa Jokate alikuwa pia akienda mikocheni alipodaiwa alikuwa nakaa Dimpoz sababu ya penzi kukolea.

Hata hivyo si Jokate, Ommy wala Vanessa ambaye amepatikana kuzungumzia issue hii but habari akiziona watafunguka tu.

                                                         Vanessa Mdee na Ommy Dimpoz


Read More »

Diamond "Mwaka Huu Namuoa Wema Sepetu Na Nataka Harusi Yangu Waje Mashabiki Wangu Kushuhudia, Nitaifanyia Hata Uwanja Wa Taifa"

0 comments
KUPITIA Gazeti la Mwanaspoti ambalo kwa mujibu wa takwimu za mauzo nchini ni wazi kwamba halina mpinzani, msanii wa muziki wa kizazi kipya Diamond Platinumz ametangaza ndoa na mchumba wake wa muda mrefu Wema Sepetu anayosema itafungwa hivi karibuni.

Msanii huyo ghali zaidi nchini kwa sasa, ametamka hayo alipozungumza na Mwanaspoti nyumbani kwake Sinza jijini Dar es Salaam juzi Jumatano. Alisema kuna mambo mengi yaliyomchelewesha kufikia hatua hiyo, ikiwamo maandalizi kwani amepanga mashabiki wake wahudhurie harusi hiyo.

“Ndoa ni kitu cha heri na baraka, lakini kitu kinachofanya kidogo mambo yachelewe ni kwamba sisi au mimi ni mtu ninayefahamika, kwa hiyo hata ndoa yangu watu wengi wanatamani waihudhurie,” alisema Diamond.

Pia amesisitiza kwamba ndoa si jambo la masihara kwani ni tendo la kiimani na ndio maana amekuwa makini katika mipango yake.

“Nataka kila kitu kishuhudiwe na mashabiki, ninaweza hata kuifanyia Uwanja wa Taifa,” aliongeza.

“Unajua nilishindwa kufanya mambo haya haraka kwa sababu wengi nadhani wangeamini kwamba ninafanya hivyo ili kutafuta umaarufu zaidi, tunataka tufanye kiusahihi yasije tokea mambo kama ya Instagram tunataka tuje kuwa mfano wa kuigwa.”

Alipoulizwa tarehe ya ndoa hiyo Diamond alisema: “Nilishasema ni hivi karibuni, unajua siku zote vitu vya kheri waswahili wanasema lazima uvifiche, hata Mwenyezi Mungu naye anasema anampenda mtu aliye na siri, lazima vitu vingine uvifiche ili vipate kufanikiwa. Wakati mwingine kunakuwa na husda, hasidi kwa hiyo ukiviweka wazi sana vinaweza kutofanikiwa.”

Taarifa kwamba Diamond hataoa zilisambaa na kudaiwa kumchefua mchumba wake Wema Sepetu ambapo katika mahojiano mkali huyo wa wimbo ‘Mdogo Mdogo’ alisema: “Kwanza sikuwahi kusema siwezi kuoa, nilishtushwa na gazeti hilo, nilisikitika kwa kweli na iliniuma sana, lakini nikaona nikijibu nitaonekana kwamba sina adabu, kwa sababu siku zote anayeanza huwa haonekani lakini anayemaliza. Pia siwezi kubishana na vyombo vya habari, mwisho wa siku ni watu haohao nitawategemea wanifanyie kazi zangu,” alisema.

Hata hivyo Diamond alisema mchumba wake anaumizwa na vichwa vya habari ambavyo vimekuwa mwiba kwake.

“Hata hivyo magazeti yetu tumeshayazoea jinsi yanavyoandika, wakati mwingine inakuwa kama chachandu au kufurahisha baraza,” aliongeza.

Kuhusu taarifa kwamba ameachana na mchumba wake huyo, alisema: “Hatuna tatizo watu wengi wanasema tumeachana, lakini hatujaachana na hatuwezi kujibishana.

“Sijui nikujibu nini kwa sababu kila nitakachokujibu utaona namsifia kwa sababu yule ni mchumba wangu.

Read More »

Warembo wampa kichapo boyfriend baada ya kugundua anatembea na wote wawili [Video]

0 comments
Jamaa amekua akibembea na wapenzi wawili kisirisiri. Kama unavyojua, za mwizi ni arobaini, kicheche huyu astukiwa na warembo hao, na hiki ndio kichapo kilichofuatia
Read More »

Aunt Ezekiel Afunguka Mara baada ya Diamond Kuwaponda Marafiki Wa Wema Wasiokuwa Na Muelekeo Na Wapenda Anasa, Haya Ndiyo Aliyoyasema

0 comments
Aunt Ezekiel ambaye ni Muigizaji wa filamu nchini, na rafiki wa karibu wa mpenzi wa Diamond Platnumz, Wema Sepetu amezungumzia kauli ya Diamond aliyotoa hivi karibuni kuwa mpenzi wake ana marafiki wapenda starehe na anasa.
Aunt alisema..

“Diamond alivyoongea pale hakunitaja jina, kwahiyo nikisema kwamba aliongea kwa sababu yangu nitakuwa muongo. Yeye aliongea kwa niaba ya watu ambao wako na Wema, hata kama angekuwa amenitaja jina sidhani kama angeongea kwamba yule mtu anafundishwa,” amesema Aunt. “Wema ni mtu mzima anaishi mwenyewe na ana maisha yake sidhani kama ni mtu wa kufundishwa. Wema ni mtu ambaye ana maamuzi yake, watu hawajui kuna wakati wa kazi na kuna wakati wa kuspend maisha. Kwahiyo mimi na muda wangu wa kazi na nina muda wangu waku spend.”

“Sihitaji kuangalia kuna mtu anafuatilia maisha yangu kwamba eti nakuwaga na Wema. Hawanisaidii chochote. Nachotakiwa kuangalia nafanya kazi zangu na maisha yangu yanaenda mbele na sitaangalia watu wanasema nini. Mimi nina kazi zangu. Sijui kama Wema kama anahitajika kubadilika kwa sababu Diamond ndiyo anajua mapungufu ya Wema na Wema anajua ya Diamond.”

Kwa upande mwingine muigizaji huyo amesema anakuja na filamu yake mpya iitwayo ‘Mwajuma Nipe’.

Read More »

AY kuachia ngoma aliyomshirikisha Sean Kingston, kuiachia kimataifa

0 comments
Msanii AY anatarajia kuachia nyimbo mbili za kimataifa mwezi November mwaka huu. Miongoni mwa nyimbo hizo ni pamoja na ule aliomshirikisha Sean Kingston.Akiongea na kituo cha redio cha Nuru FM cha Iringa hivi karibuni, AY alisema miezi ya hivi karibuni amekuwa akiachia nyimbo kwaajili ya soko la ndani ukiwemo ‘Asante’ na wimbo mwingine atakaoutoa hivi karibuni. Alidai kuwa baada ya nyimbo hizo ndipo atakaporejea tena kwenye nyimbo kwaajili ya soko la kimataifa.

Katika hatua nyingine AY amekiambia kituo hicho kuwa yeye na Diamond watawekeza kufanya video ya wimbo mpya wa Chidi Benz, ‘Mpaka Kuchee’ walioshirikishwa.

“Watu wategemee video nzuri ya Chidi Benz,” alisema.

Read More »

NOMA SANA: DJ FETTY WA CLOUDS FM AGEUKA BONDIA, AZITWANGA KAVU KAVU AKIWA UKUMBINI..!! TAZAMA HAPA

0 comments
Mtangazaji wa Clouds Redio na TV, Fatuma Hassan ‘DJ Fetty
MTANGAZAJI wa Clouds Redio na TV, Fatuma Hassan ‘DJ Fetty’, juzikati alijikuta akitwangana makonde na mrembo mmoja ambaye jina lake halikuweza kufahamika mara moja baada ya kupishana kauli kwenye ukumbi mmoja wa starehe pande za Kahama, Shinyanga.
Katika tukio hilo, Fetty aliyekuwa kwenye ‘tour’ ya Serengeti Fiesta alizama ukumbini hapo usiku na baada ya muda mfupi paparazi wetu alishangaa kumuona akizichapa na mrembo huyo ikidaiwa walizinguana, hata hivyo waliamuliwa kabla mambo hayajawa mabaya. 
Ziara ya Tamasha la Fiesta kesho itahamia Tanga ambapo wasanii kibao wataangusha burudani ndani ya Uwanja wa Mkwakwani.

Read More »

MASIKINI..!! MSANII MWINGINE WA BONGO MOVIE YU MAHUTUTI HOSPITALINI, MAOMBI YENU YANAHITAJIKA...!!

0 comments
MUIGIZAJI aliyelamba tuzo ya Muigizaji Bora wa Kike katika Tamasha la Zanzibar Festival Film ‘ZIFF’ mwaka huu, Esha Salim Buheti hali yake siyo nzuri na anahitaji maombi ili apone kutokana na kusumbuliwa na tatizo la uvimbe kwenye kizazi.

Mwigizaji, Esha Salim Buheti akiwa hoi kitandani.
Akizungumza na Ijumaa lililokwenda kumjulia hali katika Hospitali ya TMJ iliyopo Mikocheni jijini Dar, Esha alisema, alifikishwa hospitalini hapo juzi Jumatano akiwa na hali mbaya kufuatia ‘kuendesha’ ile mbaya. 

“Nilifikishwa hapa nikiwa na hali mbaya, nilikuwa ‘naendesha’ sana hadi kufikia hatua ya kuishiwa nguvu, ilibidi wanichukue vipimo ili kujua tatizo.
Akihudumiwa Hospitalini.
“Baadaye wakaniambia nina uvimbe kwenye kizazi na UTI, yaani dah! Naomba Mungu anisaidie na naomba mashabiki wangu pia waniombee nipone,” alisema Esha.

Read More »